FRIDAY XO : UKIYAONA HAYA UJUE HANA MPANGO WA KUDUMU NA WEWE KATIKA MAPENZI YENU


Mambo mengi yanatokea katika mahusiano ya mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke. Yapo mengi hufanyika yakuchukiza na kufurahisha katika mahusiano lakini jambo ambalo limekuwa la heri kwa wote ni kuwa pamoja katika mahusiano yao kwa maisha yote, lakini kabla kukubali kuolewa wasichana au wanawake ni muhimu kuyajua haya.

1.Mwanaume anaekimbilia suala la kukuoa kabla hamjafahamiana huyo hakufai kwasababu kuna vitu ataki uvijue kutoka kwake na anaamini ukivijua hutokubali kuolewa nae.

2.Hatokuwa mwepesi kwenye kukushirikisha kwenye siri zake, hii inatokana na imani ndogo aliyonayo juu yako lakini kutokuwa na imani kunasababishwa na kukosekana kwa mapenzi ya dhati juu yako.

3.Mwanaume ambae hataki muwe karibu na hata mkiwa karibu mara nyingi anatengeneza distance kati yenu, hii ni kutokana na kutokujali uwepo wako.

4.Kutokuwa na maelewano mazuri na watu waliomzunguka iwe ni majirani au familia yake.

5.Mwanaume mvivu hafai kuwa mume kwasababu anakosa upeo wa kuwaza kuwa anatakiwa kufanya kazi kwaajili mahitaji ya familia yake.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.