HAKUNA UCHAWI JUU YA MAFANIKIO YA DIAMOND PLATNUMZ... SIRI NI HII HAPA

    Image result for diamond platnumz

Cocacola pamoja na kuwa kinywaji na brand maarufu duniani,  inaendelea kumwaga fedha nyingi kwaajili ya matangazo?

Kampuni hiyo hutumia zaidi ya dola bilioni 3 duniani kote kwaajili ya matangazo kila mwaka. Kwanini sasa wanahitaji fedha nyingi kiasi hicho kujitangaza wakati kila mmoja katika dunia hii anaijua Coca-Cola?
Ni hivi – matangazo hayakukumbushi uende kununua soda pale unapokuwa na kiu – lahashaa! Kazi yake ni kuhakikisha jina lake linakaa zaidi kichwani kwako, na ni jina ndilo unalolinunua. Kwahiyo watahakikisha wanajitangaza ili ile nembo ya Coca-Cola ikae daima kichwani kwako.
Promo kwa msanii ni kama tu ilivyo matangazo kwa makampuni kama Coca-Cola. Kwahiyo Diamond anafanya kile kile makampuni makubwa yanafanya – kuhakikisha anaijenga brand yake kwenye mawazo yako kiasi ambacho huwezi kumsahau wala kumkwepa.
Hii ndio maana hata video zake zimekuwa zikipata views nyingi kwa muda mfupi na kuwazidi wasanii wengi wakubwa wa Afrika ambao huwa hawasumbuki kupiga promo kubwa kwa nyimbo zao.
Hivyo, ni sahihi kumuita Diamond supastaa anayeutreat muziki wake kama underground. Licha ya ukubwa alionao, staa huyu bado anauchukulia muziki wake kwa mtazamo ule ule msanii mpya huwa anakuwa nao – kwamba hakuna anayenijua hivyo nahitaji kuisukuma zaidi kazi yangu.
Image result for diamond platnumz
Mfano, tangu video yake ya Salome imetoka, ameshapost kwenye Instagram (followers milioni 2.8) picha au video zinazoipromote ngoma hiyo zifikazo 39, katika kipindi cha siku 7 tu! Katika kipindi cha siku 7, ameshapost Facebook (likes milioni 1.6) kupromote wimbo huo, mara 28. Anafanya hivyo Snapchat, anafanya hivyo Twitter pia – kila siku.
Video ya P-Square, Bank Alert imetoka Septemba 18 na sasa hivi na views milioni 1.58, nyuma ya Salome yenye views milioni 2.3 na huku ilitoka siku 2 mbele. Tangu muda huo, Peter Okoye mwenye followers milioni 1.8 Instagram, ameweka post za kuupromote wimbo huo 6 tu!
Simaanishi kuwa kila msanii Afrika anapaswa kufanya kama anavyofanya Diamond, bali nakuonesha jinsi gani anavyochukulia kazi yake kwa mtazamo sawa kama ambavyo kampuni kama Coca-Cola inafanya. Kwamba licha ya ukubwa walionao, wanafanya kazi kwa mtazamo kuwa hakuna anayewafahamu. Ni ngumu kuchuja kwa msanii au kampuni yenye mentality hii.



BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA WIMBO WA SALOME - WIMBO UNAOFANYA VIZURI WA DIAMOND FT RAYVANNY

Image result for diamond ft rayvanny - salome




No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.