SAIDA KAROLI AKIRI DIAMOND AMFANYA AZALIWE UPYA KWENYE MUZIKI BAADA YA KURUDIA WIMBO WA " SALOME "

saida-karoli
Saida Karoli amekiri kuwa kabla ya Diamond kuurudia wimbo wake, Salome, vyombo vya habari vilikuwa vimemtupa kulee – vichache tu vilivyokuwa vinakumbuka hata kama yupo hai, kwa mujibu wa maelezo yake.
“Vyombo vya habari vilikuwa vimeshanisahau, leo hii vinanitafuta,” anasikika akisema Saida kwenye kipande cha sauti alichokiweka Diamond Instagram.
“Ndugu zangu baadhi wanajua hata sipo duniani, leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta, kwakweli nimefunguka, najihisi kuzaliwa upya,” alisema.
Maria Salome ulikuwa wimbo wenye mafanikio makubwa kwa Saida Karoli. Pamoja na kumlipa kwa kuurudia wimbo huo, Diamond amesema asilimia 25 za mapato ya wimbo huo yataenda kwa Saida.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.