WATU 12 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI LA NEW FORCE MKOANI NJOMBE +PICHA



Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa.







No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.