FIESTA 2016 LAKANUSHA UWEPO WA MSANII KUTOKA MAREKANI JAY Z KATIKA TAMASHA HILO DAR NOVEMBER 5



Image result for jay z
Fiesta 2016 limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba watamleta msanii wa Marekani Jay Z katika show ya Fiesta Dar es salaam.
Mapema Jumamosi hii zilisambaa picha ‘fake’ inayomuonyesha msanii huyo mahiri duniani akiwa ameshasajiriwa kwa ajili ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 5 katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Clouds FM umetoa taarifa hii:
Kumetokea uzushi kwamba tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo #November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; picha iliyotengenezwa kueneza habari hiyo ni batili
Wasanii wakimataifa ambao tayari uwepo wao umetangazwa ni pamoja na Yemi Alade wa Nigeria, Jose Chameleone wa Uganda pamoja na Tekno wa Nigeria.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.