FRIDAY XO : UNAYAJUA MAUMIVU YA MAPENZI ??

#friday XO

Hakuna mwenye moyo ambaye anafurahishwa na maumivu katika mapenzi. Hapa nazungumzia usaliti, unyanyasaji, masimango na mengine mengi katika uhusiano wa kimapenzi.

Wapo watu ambao ni wa kwanza kuwaumiza wenzao lakini wao wakiumizwa ni matatizo tupu! Wanajihisi kama wao pekee ndiyo wenye moyo wa kuumia lakini wenzao hawapati maumivu. Hivi hii inaingia akilini kweli?

Siku zote lazima ufahamu kwamba mioyo yote ina nyama. Kuna mambo mengi ambayo mpenzi akifanyiwa na mwenzake lazima ataumia sana. Ingawa kuna mengine yanafichwa au kupasishwa kama sahihi, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba yanaumiza.

Image result for love hurts images

Kikubwa ambacho unatakiwa kufahamu ni kwamba maumivu hayo yapo sawa kwa kila mmoja. Haijalishi jinsia, umri, kabila wala dini, maumivu ya mapenzi yote yanafanana. Kufanana huko kunasababishwa na mioyo yote kuwa na nyama!

Kwa sababu mioyo yote ina nyama basi unatakiwa kufahamu kwamba, jinsi unavyoumia wewe moyoni mwako, ndivyo mpenzi wako anavyoumia ikiwa utamfanyia makosa kama ambayo unamfanyia wewe.

UMEWAHI KUWAZA KUHUSU KUSALITIWA?

Unajua kabisa una mpenzi, tena inawezekana wakati mwingine mmeshawahi kuzungumza juu ya kuishi pamoja, lakini bila haya wala aibu, unamsaliti! Kwa nini unafanya hivyo? Kama umeona hana thamani tena kwako, kwa nini unazidi kumpotezea muda?

Image result for love relationships conflicts

Unafikiri anafurahia sana wewe kuwa na kimada mwingine huko uchochoroni au unadhani atafurahia siku akijua kuwa una mtoto umezaa nje ya ndoa yako? Nafsi yako yenyewe inakusuta, inajua ni kiasi gani unamkosea mpenzi wako lakini unajifanya kichwa ngumu na kuendelea na uchafu wako. Kwa nini hutaki kubadilika?

Hebu jitoe katika nafasi yako, kisha mfanye mpenzi wako ndiyo wewe, halafu fikiria kama yeye ndiyo angekuwa anakusaliti, ungejisikiaje? Lazima utaumia! Sasa kama utaumia kwa nini unaendelea kumfanya mwenzako akose raha?

Lazima uwe na moyo wa huruma, akili yako ifanye kazi ipasavyo na kugundua makosa unayoyafanya kisha kufanya mabadiliko ya haraka. Amini jinsi utakavyoumia kwa kufanyiwa mabaya na mwenzako ndivyo mpenzio anavyoumia kwa mabaya unayoyafanya. Wengi wamekuwa wakiwasaliti wapenzi wao wakiwa hawafikirii siku ya wao kufanyiwa hivyo itakavyokuwa.


JIUNGE NASI, KILA IJUMAA KATIKA FRIDAY XO ... NJOO TUJIFUNZE JINSI YA KUIMARISHA MAHUSIANO YETU 

#friday XO

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.