IMPORTANT !!! TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MKOPO ELIMU YA JUU KUTOKA BODI YA MIKOPO ( HESLB)



Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.
 
Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.
 
NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.