MAJINA 30 YA WACHEZAJI WATAKAOWANIA TUZO YA BALLON D' OR 2016

ballon-dor-2016

Tangu mwaka 2010, tuzo ya Ballon D’Or na mchezaji bora wa mwaka wa FIFA zimeunganishwa na kuwa tuzo moja ‘FIFA Ballon D’Or’.
Rais mpya wa FIFA Gianna Infantino amesema anataka kuirejesha tuzo ya shirikisho hilo linalosimamia soka duniani ili kuongeza thamani ya shirikisho, kwahiyo safari hii kunauwezekano kukawa na tuzo mbili tena.
Wachezaji wawili wa Manchester City Sergio Aguero na Kevin de Bruyne pamoja na mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic pia wamo kwenye list hiyo.
Jarida la France Football limetoa orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo kwa magroup ya wachezaji watano-watano.
Tuzo hiyo ambayo hutolewa na jarida la France Football kila mwaka tangu mwaka 1956, lakini kwa miaka sita iliyopita ilikuwa ikijulikana kama Fifa Ballon d’Or ikitolewa kwa kushirikiana na shirikisho la soka duniani.
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita huku akiweka rekodi ya kuitwaa kwa mara ya tano.
Wachezaji wa tano kutoka ligi ya England – wachezaji watatu kutoka Man City Yaya Toure, Aguero na De Bruyne, mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na Eden Hazard wa Chelsea walikuwa miongoni mwa wachezaji  23 walikuwepo kwenye list mwaka uliopita, pamoja na Bale ambaye ni raia pekee wa Uingereza.
Mara ya mwisho mchezaji tofauti na Messi na Ronaldo kutwaa tuzo hiyo ilikuwa ni mwaka 2007, ambapo kiungo mchezeshaji wa AC Milan wakati huo Ricardo Kaka aliposhinda tuzo hiyo.
Ibrahimovic na mchezaji mwenzake wa Manchester United Paul Pogba pia walikuwepo kwenye list kutokana na viwango vyao wakati huo wakiwa kwenye klabu zao za zamani Juventus na Paris St-Germain.
Orodha hiyo imekuwa ikichujwa hadi kufikia wachezaji watatu kabla ya tuzo kutolewa mwezi January.
List ya majina ya wachezaji wanaowania Ballon d’Or 2016 : 
Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Levandowski (Bayern Munich), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Riyad Mahrez (Leicester City), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Dimitri Payet (West Ham), Pepe (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Rui Patricio (Sporting Lisbon), Sergio Ramos (Real Madrid), Luis Suarez (Barcelona), Jamie Vardy (Leicester City), Arturo Vidal (Bayern Munich).

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.