MTOTO MCHANGA AZALIWA MARA MBILI BAADA YA UPASUAJI
Mtoto mchanga wa kike kutoka Lewisville, Texas, 'amezaliwa' mara mbili baada ya kutolewa katika kizazi cha mamake kwa dakika 20 ili kufanyiwa upasuaji.
Akiwa miezi minne mja mzito, Margaret Hawkins Boemer aligundua kuwa binti yake, Lynlee Hope, ana uvimbe katika uti wake wa mgongo.
Uvimbe huo unoajulikana kama sacrococcygeal teratoma, ulikuwa unasukuma damu kutoka kwa mtoto huo - jambo lililoongeza hatari ya moyo wa mtoto huyo kutofanya kazi.
Baby Lynlee alikuwana uzito wa chini ya kilo moja wakati wapasuaji walipomtoa kwenye uzao wa mamake.
Bi Boemer awali alikuwa amebeba mimba ya pacha, lakini alimpoteza mtoto mmoja kabla ya kumaliza miezi mitatu ya kwanza. Awali alishauriwa kuitoa mimba hiyo kabla ya madakatari wa wa hospitali ya watoto ya Texas Children's Fetal Center kumpndekezea upasuaji huo wa hatari.
Uzito wa uvimbe huo na ule wa mtoto ulikuwa karibu sawa wakati upasuaji ulipofanywa. Aliarifiwa kuwa mwanawe Lynlee ana asilimia 50 ya kufanikiwa kuishi.
Lynlee Boemer alitolewa kutoka uzao wa mamake kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha yake.. kabla ya miezi mitatu baadaye kuzaliwa kupitia upasuaji. |
Bi Boemer aliambia CNN: " nikiwa na miezi mitano, uvimbe huo ulikuwa unasitisha moyo wake kufanya kazi, kwahivyo ilikuwa ni uamuzi baina ya kuruhusu uvimbe huo ummalize au kumpa nafasi ya kuishi.
"Ulikuwa uamuzi wa rahisi kwetu: Tulikuwa tunataka kumpa maisha."
'Moyo wake ulisiti kupiga'
No comments:
Post a Comment