MATATIZO YA AKILI YANAYOMKUMBA KANYE WEST YAMPA HASARA YA DOLA MILLION 30

Image result for kanye west

Kanye alisitisha ziara yake saa sita kabla ya kufungwa pingu na kupelekwa hospitali ya UCLA Medical Center kwa uangalizi wa tatizo la akili.
Rapper huyo anadaiwa hajapoteza tu takriban dola milioni 30 kwa kukatisha show zilizokuwa zimesalia za ziara hiyo, bali pia anadaiwa fedha za kumbi na gharama zingine kibao za maandalizi.
Tovuti ya TMZ imedai kuwa Kanye alikuwa amefungua bima ambayo inamlinda iwapo ataugua na kushindwa kuendelea. Bima hiyo inahakikisha Kanye analipwa si tu fedha ambazo angeingiza, bali pia fedha alizotakiwa kuwalipa watu wengine iwapo kutatokea tatizo.
Hata hivyo, watu wa bima wanaweza kukataa kumlipa iwapo Kanye alikuwa na tatizo ambalo hakuwaambia kabla au kama tukio hilo lilitokea katika mazingira ya yasiyoeleweka.
Kanye alilazwa hospitali Jumatatu Nov. 21 kutokana na uchovu na kukosa usingizi.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.