NANI MKALI ? - CHRISTIAN BELLA VS BANANA ZORO, MSHINDI KUONDOKA NA MIL 50 ZA MAKONDA

page

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema ataandaa show ya kuwashindanisha kuimba live kati ya waimbaji wawili mahiri, Christian Bella na Banana Zoro na mshindi mmoja kati yao ataondoka na kitita cha tsh milioni 50.

Amesema hayo katika hafla fupi ya kuwashukuru watumishi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika ziara yake ya siku kumi ya kusikiliza kero za wananchi na pamoja na kuzitatua.
RC alisema yeye ni mpenzi wa muziki wa live hivyo anawataka wasanii hao kukaa pamoja na kujadiliana ni lini watafanya show hiyo ili maandalizi yaanze kufanyika mapema.
“Hakuna mshindi wa pili wala watatu, tunamtaka mmoja tu ambaye ataondoka na milioni 50. Kwa hiyo pangeni muiangalie ni lini mtafanya hiyo show,” alisema Makonda.
Pia Makonda walitoa zawadi mbalimbali kwa baadhi ya watumishi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali ambao alionyesha kufanya kazi vizuri katika ziara hiyo.
Katika halfa hiyo Banana Zoro, Christian Bella, Mrisho Mpoto ni miongoni mwa wasanii ambao walitoa burudani.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.