PEP GUARDIOLA : NI NGUMU KUWA MCHEZAJI SOKA MZURI KAMA HAUFANYI MAPENZI NA MWENZI WAKO

Image result for pep guardiola

Samir Nasri alisema kitu ambacho kili make headline kubwa wiki hii kwamba manager Pep huwa anawambia wachezaji wafanye mapenzi kabla ya usiku wa manane ili wapate muda mrefu wa kupumzika.
Nasri sasa hivi yupo kwenye mkopo Sevilla na hana dalili za kurudi City. Mambo mengine ambayo yapo wazi ni kwamba Pep alikata internet access kwenye eneo la mazoezi la Manchester City ili wachezaji waweze kuongea wao kwa wao na kuacha kutumia simu zao kwa muda mrefu.
Kuhusu kufanya mapenzi mapema kabla ya usiku wa maneno sio kocha wa kwanza kuwa na imani hizo. Makocha wengi wanaamini kwamba kufanya tendo hilo mapema badala ya asubui humfanya mchezaji kuwa na nguvu za kutosha akiwa uwanjani.
Kwenye mkutano wa waandishi wa habari bila kupoteza nafasi waandishi wa habari walimuuliza kocha Pep kuhusu maneno hayo ya Nasri. Jibu la Pep kuhusu yeye kuwaagiza wachezaji kufanya mapenzi mapema alijibu kwa mkato na kuendelea kuacha maswali mengi.
Pep alisema,“Ni vigumu kwa mchezaji kuwa mchezaji mzuri uwanjani kama hafanyi mapenzi na mpenzi wake”. Pep alitoa maneno hayo akicheka na kuendelea na maswali mengine.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.