PICHA: UTAFITI UNAONESHA KWAMBA PANYA WANAPENDA SANA KUCHEKA

PANYA


Amini usiamini panya ni kiumbe wa ajabu ambaye wengi humhofia kutokana na tabia yake ya kung’ata na kupuliza; ni kiumbe pekee anayeweza kukung’ata na maumivu yake ukaja kuyasikia baadae kabisa. Lakini si hilo tu pia kiumbe huyu huogopwa kwa uchafu na hasa ugonjwa wa tauni.

Lakini tofauti na unavyofikiri panya ni mnyama wa kupendeza kwani utafiti mpya umebaini wanapenda sana kucheka. Watatifi kutoka Chuo Kikuu cha Humboldt cha Ujerumani wamegundua ubongo wa panya una neva inayohusiana na vitendo vya kucheka.


PANYA

Shimpei Ishiyama na Michael Brecht wamepima shughuli za neva husika kwenye ubongo wa panya na kutafiti mabadiliko ya shughuli hizo kabla na baada ya kuwashwa. 

Utafiti unaonesha panya wakiwashwa, wanacheka sana na kucheza dansi kama waliofurahishwa, na inaonekana kwamba hata panya wanajua mikono ya binadamu itawawasha. 

Lakini vicheko vyao ni vya ‘ultrasonic’ na havisikiki na binadamu. Kabla ya hapo wanasayansi walifikiri neva hizi zinahusiana na hisia ya kugusa tu, lakini utafiti huo mpya unaonesha kuwa neva hizi pia zinahusiana na hisia ya furaha.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.