SERIKALI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KUFUATILIA WANAOCHAGULIWA KUWA VIONGOZI KATIKA VYUO VIKUU NCHINI

1-3-640x360

Serikali imesema itakuwa makini katika uteuzi wa viongozi wanaostahili kushika nyadhifa mbalimbali vyuo vikuu.

Taarifa hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Muhandisi Stella Manyanya, wakati akijibu swali bungeni Alhamis hii mjini Dodoma.
Swali hilo liliuliza: Je, nini msimamo wa serikali kuhakikisha kada za watumishi wa umma zinaheshimika?”
Majibu ya Mhandisi Manyanya yalikuwa:
“Uteuzi wa kada za waendeshaji pamoja na wakuu wa idara na vitengo katika vyuo vikuu vya umma kufuata muundo wa utumishi wa wafanyakazi waendeshaji ambao pamoja na mambo mengine unazingatia miongozo inayotolewa na serikali kupitia msajili wa hazina na ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora.”
“Nina imani kwamba tatizo si taratibu sheria au miongozo iliyopo ya uteuzi kama hati idhini ya vyuo vikuu yaani university charter, bali ni ukosefu wa maadili na ubinafsi kwa baadhi ya wahusika kwenye michakato hiyo."
 Serikali imeshachukua hatua ya kuchunguza malalamiko kama hayo katika vyuo na taasisi chini ya wizara ya elimu sayansi na teknolojia ili kujua ukweli ili ikibainika kuwa kuna wahusika walivuruga utaratibu na kupelekea kuteuliwa viongozi wasio stahili watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.