JIBU ALILOLITOA LADY JAY DEE BAADA YA KUAMBIWA KWANINI ASIWE ANAVAA MADELA KWENYE VIDEO ZAKE

Image result for LADY JAY DEE

Weekend hii Lady Jay Dee aliungana na wasanii wenzake wanaowania Tuzo za EATV kufichua siri ya mafanikio yao mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani), huku wakiwataka wanafunzi hao kuuliza baadhi ya maswali.

Moja kati ya swali ambalo aliulizwa muimbaji huyo na mmoja kati ya wanafunzi wao, kwanini anavaa nguo zisizo na maadili kwenye video zake wakati wanaweza kuvaa nguo za madela ambazo amedai ni za heshima.
Katika kujibu swali hiyo, Lady Jay Dee alisema yeye binafsi  hawezi kuvaa madela na ni nguo ambayo haipendi kuvaa.
“Mimi sipendi kuvaa madela kwa hiyo siwezi kuvaa dela kwenye wimbo wangu,” alisema Lady Jay Dee “Na mimi naamini sanaa unafanya kile kitu ambacho uko huru nacho na unakifanya kutoka moyoni,”
Pia muimbaji huyo amesema yeye anaamini mashabiki wake wanampenda vile anavyofanya ndio maana mpaka sasa anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wake.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.