TRUMP AMTIMUA MWANASHERIA MKUU KWA KUPINGA AGIZO LAKE LA KUZUIA WAHAMIAJI, OBAMA AVUNJA UKIMYA

Marekani

Ofisi ya rais wa zamani wa Marekani Barack Obama imetoa tamko na kusema kwamba raisi huyo wa zamani anakerwa na maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga tamko la raisi Donald Trump kutaka kuweka vizuizi vya uhamiaji juu ya wasafiri kutoka kwa baadhi ya nchi za Kiislamu.

Msemaji wa rais Barack Obama, Kevin Lewis, amesema kwamba raisi mstaafu kimsingi hakukubaliana na wazo la ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya dini yao.

Na kuongeza kusema kwamba wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kusikilizwa na viongozi waliochaguliwa na ndiyo matarajio yao pindi Marekani inaingia hatarini .
Kaimu mwanasheria mkuu wa Marekani Sally Yates
Kwa nyakati nyingine, Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.
Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.