SIMBA SC : TUMECHOKA KUONEWA NA TFF
Wakati Maamuzi ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ikitarajiwa kulipua bomu muda wowote kutoka sasa juu ya hatma ya pointi tatu na mabao matatu waliyopewa Simba kufuatiwa malalamiko yao, Uongozi wa Simba umekuja juu na kuishutumu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Sakata hilo limeendelea kushika hatamu .kutokana na Kamati hiyo kupokea barua ya kukata rufaa kutoka timu ya Kagera kupinga maamuzi ya kamati ya saa 72 kuipoka timu hiyo pointi na kuwapa Simba.
Katika maamuzi ya kamati hiyo iliyokaliwa jana ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wa TFF Selestine Mwesigwa na kuita mashahidi akiwemo mchezaji husika Mohamed Fakhi, Mwamuzi wa mezani katika mchezo huo wa African Lyon dhidi ya Kagera Jonesia Rukyaa, waamuzi wa pembeni pamoja na Meneja wa Kagera Mohamed Husein.
Kufuatia hilo, Uongozi wa klabu ya Simba umesema hakukuwa na haja ya Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili marejeo (Review) ya shauri la timu ya Kagera Sugar kwa madai kuwa haina uhalali huo.
Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Kamati hiyo kukutana jana kwenye Hotel ya Protea kupitia shauri hilo ambapo mpaka sasa bado maamuzi yake hayajatangazwa.
Ofisa habari wa Simba Hajji Manara ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari kuwa licha ya kutokuwa sahihi kwa Kamati hiyo kuketi kwakua suala hilo lilitakiwa lipelekwe bodi ya ligi lakini pia kwa mujibu wa sheria za nchi shauri la mrejeo halipaswi kufanyika kwa kuita mashahidi wapya kama ilivyotokea jana.
Manara amesema haijawahi kutokea duniani kote kuwa mtuhumiwa anaitwa kwenye Review au mwamuzi wa nne (Fouth Official) ambaye hata haandiki ripoti anaitwa kutoa ushahidi kwenye kamati jambo ambalo halijawahi kutokea na zaidi ameitaka TFF kutenda haki kwani wamechoka kuonewa. "TFF endapo watashindwa kupata haki yao suala hilo litafika mbali kwa maelezo kuwa tumechoka kuonewa kwani mara nyingi wamekuwa wakiipendelea Yanga,"
Manara amemshutumu Rais wa TFF Jamal Malinzi kuwa Wanafahamu kinachoendelea kati yake na mwamuzi Donisia Rukyaa na wanao ushahidi wa kutosha kuhusu wao.
No comments:
Post a Comment