MASHABIKI WA SOKA KENYA WAITAMANI EVERTON FC

Leo Tarehe 31 Mei, 2017 jessengoty.com tumekuletea Habari kubwa kabisa inayotrend sasa katika mitandao tofauti ya kijamii. Ni ile inayohusu mashindano ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SPORTPESA ambapo timu nane zinazodhaminiwa na kampuni hiyo kutoka nchi za Tanzania na Kenya watachuana vikali.

Michuano ya SportPesa Super Cup, imeanza kuwa gumzo huku Wakenya wakitamba zaidi kuwa wanataka timu yao ichukue ubingwa na kupata nafasi ya kucheza na Everton ya England.

Bingwa wa michuano hiyo atapata nafasi ya kucheza na Everton kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tayari makundi mawili ya SportPesa Super Cup yametangazwa na yatajumuisha timu za Tanzania Bara, Visiwani na Kenya.

Timu kutoka Tanzania ambao ni wenyeji ni Simba, Yanga, Singida United na Jang'ombe.

Wakati kutoka Kenya ni Gor Mahia, Express na Nakuru All Stars.

Makundi ya michuano hiyo yako hivi; Kundi la kwanza linakwenda kwa mfumo huu, LEopards wanatcheza na Singida na Yanga itawavaa Tusker. Mshindi wa kila upande watakutana kucheza nusu fainali na mshindi atakwenda fainali.

Kundi la pili, Gor Mahia atawavaa Jang'ombe na Simba itakuwa dhidi ya Nakuru. Washindi watakutana kucheza nusu fainali na mshindi atakwenda fainali.

Mashabiki wengi wa soka kutoka Kenya wamekuwa wakiandika mitandaoni kutoa maoni wakizisisitiza hasa Gor Mahia na Leopards kulinda heshima ya Kenya na kupata nafasi hiyo ya kucheza na Everton.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.