" USHAURI ELEKEZI UJENZI WA BARABARA SERENGETI UZINGATIE MASLAHI YA WATANZANIA " - RC GAMBO
Mkuu wa Mkoa Arusha, Mh. Mrisho Gambo amewataka wadau wanao husika na upembezi yakinifu wa barabara kuu kupitia kusini mwa mbuga ya serengeti ( Serengeti south bypass) kuzingatia maslahi ya mapana ya kitaifa, kiuchumi, na kuhifadhi barabara hiyo ili iweze kuleta tiji kwa vizazi vijavyo.
Mh. Gambo alisema " Hata kama hizi fedha zinatolewa na wajerumani ni muhimu wataalam wetu wakawa macho ili maamuzi yasiyumbishwe kwa kutegemea maslahi ya watoa fedha, ni muhimu utaalam ukawekwa mbele "
Ujenzi wa barabar hii, serikali ya Tanzania imepokea ufadhili wa fedha kutok benki ya Maendeleo ya Ujerumani ( KFW ) kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa barabar kuu kupitia kusini mwa mbuga ya Serengeti. Barabara hii itasaidia usafirishaji wa wa abiria na mizigo kwa maeneo ya kaskazini - magharibi mwa mikoa ya Arusha na Mara na pia kuongeza wingi wa magari yanayopita kwenye mbuga.
Mradii huu utapita katika mikoa sita ya kiutawala ambayo ni Arusha, Manyara, Simiyu, Mara, Singida na Shinyanga. ambapo pia katika mkutano huo alikuepo pia Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Rc Dr. Joel Bendera.
Chini ni picha za Mkutano huo uliofanyika MAY 30, 2017. Mount Meru Hotel Arusha.
No comments:
Post a Comment