FRIDAY XO : MAMBO FLANI AMAIZING YAKUFANYA ILI USIACHWE NA MPENZI WAKO

FRIDAY XO
YAFANYE HAYA ILI USIACHWE NA MPENZI WAKO. 




Onesha kwamba uko tayari kufanya jambo lolote ili kuokoa mahusiano yenu na hauko tayari kumpoteza katika maisha yako, wanawake tuna nafasi kubwa ya kuwashawishi wanaume kufanya jambo lolote.

Kubali kujishusha pale unapokosa au hata usipokosa kwa sababu wanaume huwa ni wagumu kukubali makosa yao jitahidi kutuliza hasira zake akiwa amekasirika na baada ya kutulia kwa hasira mueleweshe na atakuelewa.

Jitahidi kuwa mbunifu katika nyanja tofauti lakini haswa maswala ya kitandani maana kutokuwa mbunifu kutakufanya mpenzi wako akuchoke na kutamani muachane hata kama anakupenda lakini ubunifu muhimu.

Onyesha unajali sana maswala ya maisha yenu na sio mda wote unawaza kufanya starehe, wanaume wanahitaji mwanamke ambaye anaakili ya maisha na sio bora liende tu kuwaza bata kila wakati.

Mshauri wakati wa matatizo na zaidi matatizo yanayomhusu upande wa familia yake, wewe  ndiye kimbilio la mpenzi wako na mshauri wake mkubwa anapokuwa na mawazo.

Jitahidi kupunguza marafiki ambao hawana faida kwako, kuwa na marafiki wenye mantiki katika maisha kwa sababu wanaume wanaamini marafiki wa kike huwa wanashauriana kuhusu maswala ya kutafuta wanaume na hakuna ushauri wa maana wanaoshauriana wakikutana.

Kuwa msafi, kuanzia mazingira yanayokuzunguka na usafi binafsi wa mwili wako, mwanamke hafundishwi kuhusu suala la usafi na mwanaume anaamini akikwambia kuhusu usafi unaweza ukakasirika na ikawa sababu ya kuachana.

Epuka kumfanya mpenzi wako kitega uchumi, sisemi msiwaombe wapenzi wenu pesa hapana jitahidi awe anakupa mwenyewe kwa hiyari yake au ukimuomba iwe ni shida kubwa na isiwe mara kwa mara.

Punguza kupenda vitu vya gharama na ikiwezekana acha kabisa wanaume hawafikirii kuwa na mwanamke mwenye matumizi makubwa sana kwa kuamini siku akikosa pesa utamkimbia.

Usiongelee masuala yanayokuhusu wewe na mpenzi wako mbele ya halaiki au kwa marafiki jitahidi kuchagua marafiki wa kuwashirikisha mambo yako kwa sababu sio wote wanapenda mahusiano yako.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.