MALKIA ELIZBETH WA UINGEREZA ATIMIZA MIAKA 90, HII LEO. + HISTORIA YAKE KWA NJIA YA PICHA :" THE QUEEN REIGN"




Na Jesse Ngoty on April 21, 2016.

Malkia Elizabeth ametimiza leo miaka tisini ya kuzaliwa.Malkia atasheherekea siku hii kwa kukutana na wananchi wake katika matembezi atayafanya huko Windsor.
Malkia Elizabeth ametawala kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza, muda unaokadiriwa kufikia zaidi ya sitini na nne hadi hivi leo, 
Queen Elizabeth II, Alizaliwa mnamo April 21, 1926 huko mjini mayfair, london, United kingdom. mume wake ni Prince Philip,  duke of Edenburg, (m. 1947) , ana watoto wa nne, akiwemo Prince Charse, Princess Anne, Prince Edward na Prince Andrew. 
Hapa Tanzania, sherehe za kusherekia siku hiyo ya kuzaliwa malikia huyo inatarajiwa kufanyika ubalozi wa uingereza Tanzania, ikitegemewa kuuzuriwa na viongozi na wananchi mbali mbali. 

Happy birthday Queen Elizabeth II. 

HAPA NIMEKUSOGEZEA HISTORIA YA MALIKA HUYO KWA NJIA YA PICHA,,,

1926 – Kuzaliwa Aprili 21 Binti mfalme Elizabeth Alexandra Mary amezaliwa katika mji wa Mayfair, jijini London siku ya Aprili 21, 1926. Baba yake, the Duke of York ni wa pili katika mlolongo wa kiti cha kifalme Uingereza. Aliitwa jina la utani la Lillibet na familia yake. 1930 – Binti Mfalme Margaret azaliwa

Elizabeth apata dada yake. Familia hiyo ya kifalme ilipata mtoto wao huyo na kumuita Princess Margaret Rose 21 August, 1930 katika kasri la Glamis, nchini Scotland. 

George VI amekuja kuwa mfalme baada ya kaka yake, Edward VIII, kujiuzulu ufalme akitaka kumuoa mjane wa kimarekani. Akipewa jina la Mfalme George VI, alikuwa ni kiongozi mwenye haya

Akiwa na umri wa miaka 18, binti mfalme Elizabeth aliisaidia nchi yake katika Vita kuu ya Pili ya Dunia ambapo alijiunga na Women's Auxiliary Territorial Service akiwa kama Subaltern wa kiwango cha pili. Alifunzwa kuwa dereva wa gari la jeshi na ufundi kabla ya kujiunga na mafunzo ya ukomando miezi mitano baadaye. Ni kiongozi wa taifa anayeishi katika wale walioshiriki katika vita hivyo, WW II.

Binti mfalme Elizabeth aliolewa na Luteni Philip Mountbatten, ambaye alizaliwa katika familia ya hadhi yenye mchanganyiko wa Denmark na Ugiriki. Katika ndoa hiyo kulikuwa na keki yenye urefu wa futi 9 na wanandoa hao walipata zaidi ya zawadi 2,500. Philip, ni kiongozi wa Edinburgh, akiwa ndiyo kiongozi mkubwa zaidi katika nafasi hiyo

Elizabeth alijifungua mtoto wake wa kwanza na mrithi, Prince Charles, 14 November, 1948. Akabatizwa mwezi mmoja baadaye na siku moja baadaye katika chumba cha muziki cha kasri la Buckingham, kwa kutumia maji kutoka mto Jordan


Kufuatia kifo cha baba yake, George VI, Elizabeth anatawazwa kuwa Malkia katika sherehe zilizohudhuriwa na zaidi ya watu 8,000 katika ukumbi wa Westminster Abbey, 2 June. Zaidi ya watu milioni moja walipanga mistari katika mitaa ya jiji la London kwa heshima ya kiongozi mpya

Princess Anne anakuwa mtoto wa kwanza wa malkia Elizabeth kufunga ndoa ambapo aliolewa na Captain Mark Phillips, 14 November, 1973


Malkia alisherehemea miaka 25 ya kukalia kiti cha ufalme huku kukiwa na mlolongo wa matukio kuifanya Silver Jubilee, huku maelfu ya sehemu za mitaa zikijumuika naye katika sherehe hizi.


Katika kanisa la St Paul, Prince Charles, mrithi wa kiti cha ufalme, anamuoa Lady Diana Spencer, mwanamke anayedhaniwa kuwa malkia wake. Ndoa hii ilitajwa kuwa ya karne baada ya kushuhudiwa na zaidi ya watu 750 million duniani kote.


Malkia anaonja kile anakisema kuwa ni 'annus horribilis' (mwaka mchungu) 1992. Ndoa za Prince Charles na Prince Andrew zilivunjika, Princess Anne anaachika na sehemu kubwa ya kasri la Windsor liliwaka moto na kuteketeza mali nyingi.


Familia ya kifalme inaingia katika majonzi kufuatia kifo cha ghafla cha mtalaka wa Prince Charles, Princess Diana, jijini Paris, 31 August, 1997


Malkia anakumbwa na vifo vya watu wawili ambao ni wana familia katika mfuatano waa haraka sana. Dada yake, Princess Margaret, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 71 kufuatia kuugua sana, wakati mama yake mzazi akifariki akiwa na umri wa miaka 101.


Malkia alisherehekea miaka 50 ya umalkia mwaka 2002 ambapo kulikuwa na mlolongo wa sherehe duniani kote, ambapo inajumuisha matamasha mawili yaliyofanywa katika viwanja vya kasri la Buckingham.

Malkia alisherehekea miaka 60 ya ndoa yake na mumewe Prince Philip. Amekuwa kiongozi wa kwanza wa kifalme Uingereza kusherehekea miaka hiyo ya ndoa.



No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.