MWAFRIKA WAKWANZA KUWEKWA KWENYE DOLA MPYA YA MAREKANI DOLA 20 - ALIKUA MTUMWA ALIYEKATA MNYORORO.

Tubman

Picha ya mtumwa mmoja aliyekata nyororo na kisha kusaidia mamia ya wenzake kutoroka utumwa sasa itatumika katika noti mpya ya dola 20 nchini Marekani.
Bi Harriet Tubman atakuwa Mwafrika Mmarekani wa kwanza kuangaziwa kwenye sarafu ya Marekani.
Vilevile ndiye mwanamke wa kwanza katika kipindi cha karne moja katika historia ya Marekani picha yakwe kuwekwa kwenye dola.
Picha hiyo itabadilishwa na ile ya awali ya rais wa saba wa Marekani Andrew Jackson ambaye alikuwa akimiliki watumwa enzi hizo.
Sasa picha ya Andrew Jackson itakuwa nyuma ya noti hiyo.
Noti hiyo itaanza kutumika mwaka 2020 lakini idara ya fedha nchini Marekani imesema ni mwanzo wa kuwakumbuka na kuwaenzi waliopigania haki za kibinadamu nchini humo.
Bi Tubman alizaliwa miaka ya 1800 utumwani jimbo la Maryland. Alifariki 10 Machi, 1913 akiwa eneo la Auburn, jimbo la New York.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.