MH. RAIS MAGUFULI AMNG'OA MWINGINE APRIL 28/04






Taarifa ambayo imetoka April 28 2016 ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji ‘TIC’, Julieth Kairuki kuanzia April 24 2016.
Hatua hii imechukuliwa baada ya Rais Magufuli kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April 2013 mpaka sasa, jambo ambalo linazua maswali mengi.
Taarifa hiyo iliyotolewa imesema endapo atakuwa tayari kufanya kazi na Serikali atapangiwa kazi nyingine na Clifford Katondo Tandari atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji.
utenguzi

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.