MSN WANA MSAADA MKUBWA KWENYE TIMU YAO KULIKO BBC

sports

1 April 2016, 

El Clasico: MSN wana msaada mkubwa kuzidi BBC katika El Clasico

By, Shaffii Dauda

“Kama kila mmoja angekuwa kwenye level yangu, tungekuwa katika nafasi ya kwanza.” Cristiano Ronaldo alichukua hatua ya kuzungumzia level ya fitness ya wachezaji wenzie baada ya Madrid Derby ambayo walifungwa na Atletico, wengi walimsema kwa kutoa kauli hii, lakini ukiangalia takwimu za msimu huu kuelekea mchezo wa El Clasico jumamosi hii, kauli yake inaleta maana.
 Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez wamekuwa na msaada mkubwa kwa timu yao kuliko Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema.
Uchambuzi wa takwimu unaonyesha kwamba Luis Enrique amefanikiwa katika kuwategemea MSN katika kufanikisha malengo ya timu yake – MSN wamecheza mechi zisizopungua 23 za ligi kati ya 30 – wakati kwa upande wa BBC, Ronaldo amecheza mechi 30, Bale amecheza 16 huku Benzema akicheza 20, idadi ndogo ya mechi kuliko mchezaji yoyote wa MSN. Rafa Benitez na sasa Zinedine Zidane, iliwabidi kutafuta majawabu mengine kutokana na kutokamilika kwa BBC – Ronaldo kwa mara nyingine alikuwa sawa.
 Uwanjani, pia kumekuwepo na tofauti kubwa uwanjani kati ya MSN na BBC. Messi, Neymar na Suarez wamefanikiwa kupata nafasi ya magoli 322 kwnye La Liga msimu huu, Los Blancos wamepata nafasi 273. Safu ya ushambuliaji ya Barca ipo vizuri zaidi, ikionyesha alama zote nzuri ya kuelewana vizuri nje na ndani ya dimba.
Mpira mzuri, takwimu nzuri kwa Messi, Neymar na Suarez, watatu hawa wote wa takwimu zinazofanana, jambo ambalo linaifaidisha sana timu kwa sababu hatari inaweza kutokea upande wowote wa safu ya ushambuliaji, wakati kwa upande wa Madrid mara kadhaa wamekuwa wakilizamika kumtegemea Ronaldo.

 Ronaldo amefunga magoli mengi kuliko mchezaji yoyote, magoli 28, lakini takwimu ni nzuri kwake kwa upande wa BBC. Amepiga mashuti 191, ukilinganisha na Bale aliyepiga 61, pia Bale ana wastani mbaya wa kutumia nafasi kwa asilimia 14, wakati Suarez akiwa na wastani wa asilimia 24, wakati Neymar na Messi wakiwa na asilimia 19 na 21.
 MSN pia wamekuwa wakionyesha uwezo wao kwenye Clasico. Wote wamekuwa na viwango vizuri katika michezo dhidi ya Madrid. Messi amefunga magoli 6 katika mechi 9 zilizopita dhidi ya Los Blancos, wakati Suarez na Neymar wote wamefunga magoli matatu dhidi ya Madrid kila mmoja – Suarez, ambaye amecheza mechi 3 dhidi ya Real Madrid. Anaonekana kuwa wakati mzuri akicheza dhidi ya Madrid, tofauti na Bale, ambaye amekuwa na mchango mdogo sana katika mechi 4 zilizopita dhidi ya Barca. Ronaldo ndio mwiba mkuu wa Barcelona inapocheza na Madrid. Kama Messi, amefunga magoli 6 katika El Clasico 9 zilizopita.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.