RAIS MAGUFULI ATAFANYA KAMA KILE CHA SHEREHE ZA UHURU

BREAKINGNEWS

MH. RAIS DK MAGUFULI AFUTA SHAMRASHAMRA ZA SHEREHE ZA SIKUKU YA MUUNGANO ZINAZOFANYIKA KILA MWAKA APRIL 26.

Image result for breaking news

 Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  ametangaza kusitisha shamrashamra za sherehe za muungano april 26 kwa mwaka huu. ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani mbalimbali na hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.