SHABIKI KUJISHINDIA ZAIDI YA MILLIONI 50 LEICESTER IKISHINDA LIGI

Leigh Herber Shabiki wa Leicester 

Shabiki mmoja wa timu ya Leicester amesema kuwa ana uhakika klabu hiyo itashinda ubingwa wa ligi na kumfanya kupata zaidi ya pauni 20,000 ambayo ni sawa na Shillingi za kitanzania milioni 50.

Leigh Herbert aliwekeza 5000 baada ya kupata vinywaji kadhaa wakati wa likizo huko Newquay ,Cornwall mwaka uliopita.

"Nina furaha tele kwa sababu nina uhakika wa asilimia 100 kwamba hilo litafanyika". Alisema Leigh Herbert.


Leigh alicheza kamari hiyo kufuatia uteuzi wa mkufunzi Claudio Ranieri.''Nilifikiria kwamba atailetea kilabu hiyo kitu maalum''.
Claudio  Ranieri kocha aa Leicester


''Nilijua kwamba kutokana na uzoefu alionao kuna kitu kitafanyika''.Na kulingana na mambo yalivyo kwa sasa Leigh alikuwa na haki kuwa na matumaini.


Wachezaji wa Leicester




Iwapo timu yake itaishinda Manchester United ama Spurs ishindwe na wapinzani wake wa jadi Chelsea wikendi hii,Leicester watakuwa mabingwa na Leigh atajipatia pauni 20,000 ambayo ni sawa na Fedha za kitanzania millioni 50.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.