TUZO ZA WACHEZAJI WAKULIPWA- UINGEREZA ( PFA): RIYAD MAHREZ WA LEICESTER CITY- MCHEZAJI BORA WA MWAKA

Mahrez

Mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya chama cha wachezaji soka ya kulipwa Uingereza (PFA).
Mahrez amefunga mabao 17 na kusaidia katika ufungaji wa mengine 11 katika mechi 34 za ligi alizochezea Leicester na kuwasaidia sana kukaribia kushinda taji la ligi.
Mahrez ni raia wa Algeria.
Wachezaji soka ya kulipwa Uingereza ndio hupiga kura kuamua mshindi.
Kiungo wa kati Tottenham Dele Alli, 20, ndiye aliyeshinda tuzo ya PFA ya mchezaji chipukizi wa mwaka naye mshambuliaji Izzy Christiansen akashinda tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka
Alli
Mshambuliaji wa Sunderland Beth Mead, 20, ndiye aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa kike.
Mahrez, 25, alikuwa akishindania tuzo hiyo na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, kiungo wa kati wa West Ham United na wenzake wa Leicester Jamie Vardy na N'Golo Kant
Mahrez alipokezwa tuzo katika hoteli ya Grosvenor, London Jumapili saa chache kabla ya kufunga bao na kusaidia Leicester kulaza Swansea City 4-0.
Leicester wanahitaji kutwaa alama tano kutoka kwa mechi tatu walizosalia nazo ili kushinda ligi.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.