VIDEO: JINSI JUVENTUS ILIVYOSHANGILIA UBINWA SERIE A - WALIOUPATA MARA YA TANO MFULULIZO.
Juventus imeshinda taji la Serie A kwa mara ya tano mfululizo!
Ushindi wa bao 1-0 ilioupata Roma dhidi ya Napoli umeipa ubingwa wa Scudetto timu ya Juventus.
Juventus ilanza vibaya msimu wa 2015-16 baada ya msimu uliopita kunyakua mataji mawili na kufika hatua ya fainali ya Champions League na kupoteza mbele ya Barcelona.
Wakiwa bila ya nyota wao Andrea Pirlo na Carlos Tevez haikuwa rahisi kwao kufanya vizuri na hilo lilithibitika mwanzoni mwa msimu kabla ya kukaa sawa.
Kikosi hicho kilicho chini ya Massimo Allegri kilizinduka na kuanza kuikimbiza Napoli iliyokuwa kwenye kiwango bora mwanzoni mwa msimu, Juve waliipiga bao Napoli wiki chache zilizopita na kufanikiwa kutetea ubingwa wao.
Ukiangalia namna Juventus walivyoanza ligi, inashangaza kuona wametangaza ubingwa kukiwa bado kuna mechi kadhaa mbele.
Uwepo wa Gianluigi Buffon, Paul Pogba pamoja na ukuta imaara lakini wakati huo wakiwa na Juan Cuadrado, Paulo Dybala na Alvaro Morata ilikuwa ni sababu tosha ya wao kutwaa taji la Serie A
Taji hilo ni la tano mfululizo kwao kwenye ligi ya Serie A lakini wengi wanatamani kama Juventus ingefanikiwa kupenya mbele ya Bayern Munich kwenye michuano ya Champions League na kusonga mbele.
Video ya wachezaji wa Juventus wakishangilia ubingwa wao wa tano mfululizo kwenye Serie A
No comments:
Post a Comment