FRIDAY XO : UTAMJUAJE MPENZI LAGHAI? JINSI YA KUMJUA ASIYE NA MAPENZI YA KWELI



6 May 2016
FRIDAY XO: LOVE TIPS.

Inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, hiyo ni sumu na unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema usije ukawa miongoni mwa walio katika foleni!

Hakuna kitu kibaya kama kuwa katika foleni ya wapenzi kwa mpenzi mmoja, tena mbaya zaidi awe ni yule ambaye moyo wako umempenda kwa dhati.

Kumbuka, kuwa katika uhusiano na mtu ambaye haeleweki ni sawa na kukaribisha matatizo katika maisha yako, huna sababu ya kuishi kwa wasiwasi ukiwa hujui mpenzi wako anakuchukulia vipi.

Anza kumuwekea mitego mapema. Lakini katika mitego yako achana na simu yake kabisa, huna sababu ya kuchunguza simu yake lakini kama ni msaliti utajua tu, unafikiri atajificha mpaka lini?

UTAMJUAJE MPENZI LAGHAI?

Hapa ndipo kwenye kazi, kwa bahati mbaya sana kama ikitokea ukampenda mtu sana hata kama akifanya mabaya kiasi gani unaweza usiyaone, kama wewe ni wa aina hii unapaswa kubadilika kifikra. Muone wa kawaida, fanya uchunguzi wako polepole na kama ukiona moja kati ya mambo yafuatayo, ujue kuna kitu.

(a) Hataki ujulikane na rafiki zake
Hii ni kati ya alama walizonazo matapeli wa mapenzi, ni mtu wa kufanya mambo kwa upekee sana. Kila dakika hakaukiwi na neno nakupenda sana, lakini moyoni mwake hakuna alama hata moja ya mapenzi kwako.

Ni vigumu kumtambua mtu wa aina hii lakini chunguza kuhusu hili, hapendi kabisa kukukutanisha na rafiki zake na hata mkikutana nao kwa bahati mbaya basi hatakutambulisha na kama akikutambulisha hatakutambulisha kama mpenzi wake rasmi. Ataishia kusema ninyi ni marafiki mlioshibana!

Tangu lini mpenzi akatambulishwa kama rafiki? Mtu anapomtambulisha mpenzi wake humtambulisha kwa kujisikia furaha moyoni kwamba anamtambulisha mpenzi wake lakini inakuwaje kwako akutambulishe kama rafiki?

(b) Msiri kupitiliza
Hii ni alama nyingine waliyonayo wanaume wa aina ninayoielezea katika mada hii. Siku zote mambo yake ni kwa siri kubwa, kama mna ahadi ya kukutana, hataki muongozane, atakuambia mkutane moja kwa moja sehemu husika. Hata muda wa kuondoka atafanya kila njia ili kila mmoja aondoke mwenyewe na kama mkiondoka pamoja basi ujue ni usiku na hakuna atakayewaona.

Ikitokea akakubali kuongozana na wewe, hatapenda muongozane pamoja. Atalazimisha utangulie mbele yeye afuate nyuma, kwa nini? kwa sababu anaogopa kujulikana kuwa yeye ni mpenzi wako na kama anaogopa anakupenda kweli? Mapenzi gani hayo yanafanywa kwa siri? anakupotezea muda huyo.

(c) Hapendi ndugu wafahamiane
Mpenzi wa aina hii ni mjanja sana, kwanza kabisa atajifanya mtu mwenye ‘ubize’ sana, yote hii ni kukwepa kuwajua ndugu zako au wewe kuwajua ndugu zake! Wakati mwingine anakuwa hapendi ndugu zako na wake wakutane wakijua wazi kuwa nyie mna uhusiano, hili ni tatizo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.