RONALDO AMPA SHAVU ZIDANE KUENDELEA KUINOA REAL MADRID





Zidane ambaye alichukuwa mikoba ya kuifundisha timu hiyo mwezi Januari kutoka kwa Rafael Benitez ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Newcastel United ya nchini Uingereza.
Tangu Zidane aanze kuifundisha timu ya Real Madrid wamefanikiwa kucheza michezo 23 na kushinda michezo 18 na kuanza kuiweka timu hiyo kwenye nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa La Liga wakiwa nyuma ya pointi mbili na vinara wa ligi hiyo, Barcelona na Atletico Madrid wenye pointi sawa.
Ronaldo amesema, “Nadhani tunahisi kuwa na furaha zaidi chini ya Zidane. Tunahisi upendo wake, tunajua kwamba yupo katika kipindi cha kuzoea mazingira, lakini mambo yamemnyookea kwa haraka sana name namfurahia pia.”
“Daima nilivutiwa naye kama mchezaji, na sasa ni kocha hali kadhalika, jinsi anavyofanya mambo yake na kushughulika na wachezaji. Jinsi anavyofundisha tu ningependa aendelee kubaki Real Madrid,” aliongezea Ronaldo.
Ronaldo ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa takribani michezo mitatu kutokana na kuwa majeruhi anatarajiwa kuwepo uwanjani kwenye mchezo wa marudioano wa Uefa kati ya Madrid dhidi ya Manchester City ambao utafanyika kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu siku ya Jumatano.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.