DUBAI: WANASWA WAKIENDESHA MAGARI KILOMITA 300 KWA SAA

Polisi wanasa magari magari 81 wakiwa wanaendesha kilomita 300 kwa saa.


Idara ya polisi katika milki za kiarabu huko Dubai imekamata magari 81 ambayo yalikuwa yakiendeshwa kasi ya zaidi ya kilomita 300 kwa saa.

Hatua hii inafuatia uchunguzi katika barabara za kutoka nje ya mji ambapo wenye magari waling'oa namba za usajili wa magari hayo kisha wakashindana.

Polisi wanashuku kuwa mashindano hayo yanayokiuka sheria za barabarani mbali na kuhatarisha maisha ya waendeshaji wengine wa magari huwa yanaandaliwa na matajiri wanaomiliki magari ya kifahari.

Polisi walilazimika kutumia magari ya kifahari kuwanasa madereva hao watundu

Aid polisi wanashuku matajiri hao huweka dau kisha kuwaajiri madereva kushindana mabarabarani.

Polisi walikuwa na wakati mgumu kuwakamata washukiwa kwani waliendesha magari yao kwa kasi zaidi ya kilomita 290 kwa saa.

Polisi walimudu tu kuwatia mbaroni baada yao pia kuyatumia magari ya kifahari yanayomilikiwa na polisi.


Washukiwa hao watatozwa faini ya dola 27000 ambayo ni zaidi ya milioni 55 Tsh. kila mmoja


Wamiliki wa magari hayo wanatakriban siku 90 kulipa ada ya dola elfu 13,500 la sivyo magari yao yapigwe mnada.

Utafiti unaonesha kuwa mabwenyenye Dubai ndio wanaomiliki magari mengi zaidi ya miji mikuu ya London na hata New York.














No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.