FRIDAY XO : ULISHAWAHI KUJIULIZA KWANINI ANAKUPENDA ?? HII INAKUHUSU
Mapenzi ni kitu kizuri sana kama upo kwenye mahusiano sahihi, na mapenzi ni kitu kibaya sana kama utakuwa kwenye mahusiano yasiyo sahihi. Umewahi kujiuliza ni kwa nini uliyenaye anakupenda sana na umewahi kupata majibu ya hayo maswali?
Kama umewahi kujiuliza na kupata majibu basi ni vizuri sana kwa upande wako na kama umewahi kumuuliza hata yeye na akakupa majibu pia ni vizuri ingawa huwa inakuwa vigumu sana mtu kukupa sababu zote kwa nini anakupenda.
Ukiachilia mbali sababu zinginezo binafsi za mtu kukupenda lakini pia hizi zifuatazo ni baadhi ya sababu za kawaida tu ambazo mtu anayekupenda huwa anazo.
Unamjali >> Hakuna kitu kizuri kama kujaliwa na unayempenda na ndio kitu muhimu sana kwenye mapenzi, Ukionyesha kujali kwenye mapenzi basi hata vitu vingine vingi huenda kwenye mstari ulio salama na hufanya mapenzi yenu kuwa nyoofu siku hadi siku.
Unamtetea >> Unapoonyesha kuwa upande wa mwenzi wako kwenye kila tatizo au changamoto yeyote inayotokea basi huwa ni njia nzuri sana naya msingi kudumisha mapenzi yenu, Kuna mengi yanatokea kila siku kwenu ila jitahidi kila mara kumtetea kwa lolote mbele yake isipokuwa tu labda liwe kweli amekosea na hapo mrekebishe katika hali ya kimapenzi.
Unamsaidia >> Hiki pia ni kitu bora sana kwenye mapenzi hasa kwa kutambua kuwa mojawapo ya njia nzuri za kudumisha mapenzi ni pamoja na kusaidiana pale linapotokea tatizo lolote lile kwa mmojawapo kati yenu, Jitolee kwa kila hali kwa mpenzi wako pale anapopata shida au tatizo lolote.
Unamridhisha >> Hiki ni kitu safi sana kuwepo kwenye mahusiano ambayo kila mtu anaridhika na mwenzake. Iwe ni kwenye mambo ya kawaida au hata yale mambo ya ndani, ukiridhika na huyo uliyenaye na ukaridhika kwa kila anachokupa basi mapenzi huenda murua kabisa.
Source : NESI MAPENZI
No comments:
Post a Comment