TAHADHARI: MADAKTARI WA AFRIKA HUZIDISHA DAWA KWA WAGONJWA

Tatizo ni kubwa zaidi kwenye taasisi za kiafya zinazotengeneza faida
  

Utafiti unaonyesha kuwa madaktari wa nchi za kusini mwa Afrika wanatoa dawa nyingi zaidi ya zilizoagizwa na Shirika la Afya Duniani WHO. 

Utafiti huo uliofanywa na Chuo kikuu cha London kwa ushirikiano na kituo cha Kutoa ushauri wa afya cha nchini Ghana,ikihusisha nchi kumi na moja za kusini mwa jangwa la Sahara zinaonyesha kuwa wagonjwa wanapewa takribani dawa tatu kila wanapotembelea hospitali, moja zaidi ya maelekezo ya WHO.

Inasemekana tatizo ni baya zaidi kwenye taasisi zinazotengeneza faida, na kuchochea kuuza dawa.


Tafiti zimeonya kuwa matumizi makubwa ya madawa yanasababishwa na kulazimishwa kutumia dawa, kuzidisha dozi na kuleta athari mbaya kwa mchanganyiko unaosababishwa na kuchanganya dawa mbalimbali.

Pia wamegundua wagonjwa wengi wamekuwa wakipewa dawa za kutuliza maumivu pasipo kufanyiwa vipimo, na kuongeza hatari ya maambukizo yanayosababisha na kupambana na dawa.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.