UVCCM YAITISHA MAANDAMANO NCHI NZIMA AUGUST 31, YALE YA CHADEMA NI SEPTEMBER MOSI.



Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.

Hali hiyo ambayo inashangaza ni baada ya yale maandamano ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambayo wameyayapa jina la UKUTA yanatarajiwa kufanyika September mosi ikiwa yatapishana na haya waliotangaza UVCCM kwa masaa tu yaani siku moja. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo

Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa katika maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.