WACHEZAJI WAWILI (KIUNGO NA MSHAMBULIAJI) WA MANCHESTER CITY WAONDOKA KWA MKOPO


Wlifried Bonny ajiunga na Stoke City kwa mkopo
Klabu ya Stoke City imemsajili mshambuliaji Wilfried Bony kwa mkopo kutoka Manchester City.
Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27,ameanzishwa mara 15 tangu ajiunge na City kwa kitita cha pauni milioni 28 kutoka Swansea mnamo mwezi Januari 2015 , lakini hajacheza chini ya mkufunzi mpya Pep Guardiola.
Stoke pia imemsajili kipa wa Derby, Lee Grant mwenye umri wa miaka 33 kwa mkopo hadi mwezi Januari.
Wakati huohuo Beki wa Porto na Uholanzi Bruno Martins Indi mwenye umri wa miaka 24 anaendelea na mazungumzo ya kusajiliwa na klabu hiyo.
1

Manchester City pia,  wamethibitisha kiungo mshambuliaji wao Samir Nasri kujiunga na Sevilla kwa mkopo wa msimu mzima.
Awali iliripotiwa kwamba, Nasri angejiunga na miamba ya Uturuki Besiktas, lakini mwishoni kabisa Sevilla wameonekana kuwa na mkono mrefu zaidi.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Sevilla Monchi amethibitisha kwamba, Nasri ni mchezaji ambaye wamekuwa wakimfukuzia kwa muda wote kwenye dirisha hili la usajili.
Mkataba huo wa mkopo hauna kipengelea cha Nasri kununuliwa moja kwa moja endapo Sevilla watahitaji kufanya hivyo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.