KAMA WEWE NIMTUMIAJI AU MPENZI WA SIMU AINA YA SAMSUNG GALAXY, HII INAKUHUSU
Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vinavyotumia teknolojia ya umeme ya Samsung imetangaza kusitisha uuzaji wa bidhaa yake ya simu ya mkononi ya Galaxy Note 7.
Kampuni hiyo imepata taarifa kutoka nchi 10 ikiwemo Marekani na Korea Kusini zinazoeleza kuwa zimu hizo zimekuwa zikilipuka wakati wa kuweka chaji kwenye umeme huku tatizo hilo likidaiwa kuwepo kwenye betri za simu hizo.
Taarifa hiyo imekuja ikiwa ni wiki moja imesalia kabla ya mshindani wake mkuu katika soko la biashara kampuni ya Apple kuzindua toleo lake jipya la simu zaa aina ya iPhone 7.
“It is a big amount that is heartbreaking,” amesema rais wa kampuni hiyo Koh Dong-jin.
Jumatano hii kampuni ya Samsung ilisema imesitisha usafirishaji wa simu hizo kwa kampuni tatu kuu zinazosafirisha simu hizo maeneo mbalimbali duniani ili kufanya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment