CHURA IS BACK.... SASA RUKSA NYIMBO YA CHURA KUCHEZWA KWENYE RADIO NA TV
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemruhusu msanii wa muziki, Snura Anthony Mushi ‘Snura’ kuachia video yake mpya ya wimbo ‘Chura’ baada ya msanii huyo kufanya marekebisho ya video ya wimbo huo na kukubaliwa na wizara.
Aidha, katika barua ya wizara imemtaka Snura kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari ili video hiyo ianze kuchezwa.
Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.
Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar es salaam, Snura amesema anamshukuru Mh waziri Nape Moses Nnauye kwa kumkubalia ombi lake la kuiruhusu kazi hiyo kutoka.
“Mh Nape ameuruhusu wimbo wangu mpya wa Chura na video Chura kupigwa na kuonyeshwa katika vituo mbali mbali vya radio na runinga baada ya kuona video yangu mpya ya wimbo ina maadili na ujumbe ndani yake ikiwa ni kukidhi makubaliano ya awali kwamba wimbo wangu ‘Chura’ utafunguliwa pale nitakapofanya video mpya ya muziki yenye maadili ya kitanzania,” alisema Snura.
Aliongeza, “Video yangu mpya Chura inaeleza maana halisi ya neno Chura. Chura ninayemzungumzia ni mwanamke anayeruka ruka katika mahusiano kwa kubadilisha wanaume mbalimbali matokeo yake kupata magonjwa sugu,”.
Pia katika barua hiyo ya Mh Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempa onyo kali msanii huyo kutokurudia kufanya tena video zisiyokuwa na maadili ya kitanzania.
No comments:
Post a Comment