WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAANZA KUWEKEWA FEDHA ZA KUJIKIMU " BOOM "
Fedha za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini zimeanza kuingia katika akaunti zao, baada ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) kusema kuanzia Jumatano hii imeanza kuingiza fedha za wanafunzi wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa mkopo
Akizungumza na gazeti la Habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa fedha hizo zinaanza kuingia siku tofauti tofauti.
“Napenda kuwahakikishia waombaji kuwa boom limeanza kuingia leo, kwa kuwa fedha hizo zinapitia benki baadhi wanapata kesho na wengine siku zinazofuata, ila sisi tumeshatimiza wajibu wetu,” alisema Badru.
“Kuna wanafunzi kama 90 wamekosa mikopo kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa, sisi tunatoa mikopo kwa wanafunzi wanaotoka sekondari. Pia kuna wanafunzi wengine kama 6,561 hawakuomba kabisa mikopo licha ya kudahiliwa na TCU hao nao tunasema hawana sifa ya kukopeshwa,” aliongeza Badru.
No comments:
Post a Comment