JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU YAIPA SERIKALI SIKU SABA KUTOA MIKOPO


Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso), imeikomalia Serikali ikitaka wote wanaostahili kulipwa walipwe ndani ya wiki moja.

Kauli hiyo ya Tahliso imekuja kutokana kuwapo kwa malalamiko mengi ya wanafunzi kukosa mikopo.

Akizungumza baada ya majadiliano na viongozi wa vyuo 44 vikuu  nchini, mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize amesema wamekubaliana kuwa Serikali ihakikishe baada ya siku saba iwe imewapa mikopo wanafunzi wenye sifa.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.