KUELEKEA MECHI KATI YA ARSENAL VS MAN UNITED LEO, HAYA NI MAMBO YA MUHIMU KWAKO KUYAJUA

Image result for man utd vs arsenal nov 19 2016

Wikiendi hii ligi mbali mbali barani Ulaya zitaendelea, baada ya kusimama wiki iliyopita kupisha mechi za kimataifa kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi. 
Kwenye ligi kuu nchini England Manchester United itakuwa mwenyeji wa Arsenal kwenye uwanja wa Old Trafford.
Man United iliyopo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 itaingia kwenye mechi hiyo ya mzunguko wa kumi na mbili bila mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic anayetumikia adhabu. Pia itawakosa mabeki wake mahiri Eric Bailly na Chris Smalling.
Arsenal ambayo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 24 itaingia bila ya beki wake wa upande wa kulia, Hector Bellerin aliye majeruhi na kiungo Santi Cazorla.
Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya mchezo huu, je wajua kwamba?
  1. Manchester United wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya mechi kumi za hivi karibuni walizocheza dhidi ya Arsenal. Hiyo ilikuwa mwezi October 2015 ambapo United walipoteza 3-0 kwenye uwanja wa Emirate.
  1. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho hajawai kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal kwenye mechi za ligi kuu nchini England. Ameshinda mechi tano na kutoka sare mara sita.
  1. Mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Old Trafford imetoa penati kumi. Kati ya penati hizo sita zimeshindwa kuingia nyavuni.
  1. Mshambuliaji wa Man United, Wyne Rooney ameifunga Arsenal mara kumi na nne kwenye mechi zote za mashindano.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.