MAPYA YAIBUKA LIST YA WADAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO, WENGINE WASEMA HAWAKUWAHI KUSOMA CHUO KIKUU

heslb

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, imedaiwa kuwataja katika orodha ya wadaiwa sugu watu ambao baadhi yao hawajasoma Tanzania na baadhi yao wakidai kuwa washamaliza kulipa madeni yao na huku wengine wakidai kuwa hawakusoma chuo kikukuu.


Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano, Cosmas Mwaisoba amejibu maswali hayo yaliyokuwa yakiulizwa katika kipindi cha mahojiano cha JAMBO kinachorushwa na TBC1 akiombwa kutoa ufafanuzi baadhi ya watu waliowekwa kwenye orodha ya wadaiwa ambao hawahusiki na madeni hayo, Mkurugenzi huyo alijibu.
“Kuna watu ambao wamesoma nje ya nchi ambao wamekopeshwa sio kwamba kusoma nje ya nchi ndio mtu hukukopa hapana, wapo waliosoma nje ya nchi kwa kupata scolarship za nchi kadhaa ambapo bodi iliwakopesha, sasa kama kuna mtu ambaye alisoma nje ya nchi na alijisomesha mwenyewe hakupata mkopo wa bodi nadhani huyo ndiye ana haki ya kulalamika, sasa yeye atakachotakiwa kukifanya kuwasiliana nasi ili tuweze kuwangalia hiyo kesi yake ikoje akiwa na vielelezo vyake baadaye taarifa zitarekebishwa,”alisema Mwaisoba.
Bodi ya Mikopo iliwapa siku 30 wadai sugu wa mikopo hiyo kuirejesha.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.