BIRTHDAY YA BLUE IVY ( MTOTO WA JAY Z ) YAWALETA PAMOJA JAY Z, BEYONCE, KARDASHIAN... WEST ALALAMA
Couple zenye nguvu zimeunganika tena. Kim Kardashian na Kanye West waliwatembelea Beyoncé na Jay Z, nyumbani kwao, Holmby Hills, Los Angeles, Ijumaa, January 6, wiki kadhaa baada ya West kuwachana hadharani.
X17 iliripoti kuwa staa huyo wa Keeping Up With the Kardashians na mume wake, walienda kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wa Beyoncé na Jay Z, Blue Ivy aliyekuwa akitimiza miaka mitano.
Hata hivyo hawakwenda na watoto wao, North, 3, na Saint mwenye miezi 13. Kukutana kwao kumekuja baada ya West kumchana Beyoncé, 35, na Jay Z, 47, alipokuwa akitumbuiza huko Sacramento.
Katika show hiyo, Kanye alidai kuwa Queen Bey alikubali kutumbuiza kwenye tuzo mwaka jana za MTV Video Music Awards iwapo angeshinda tuzo ya Video of the Year kwa wimbo wake Formation. Kanye naye alikuwa akiwania tuzo hiyo.
West pia alimchana Jay Z kwa kutopokea simu zake baada ya mkewe kuvamiwa Paris akisema, “Jay Z, call me, bruh. You still ain’t called me. Jay Z, I know you got killers. Please don’t send them at my head. Please call me. Talk to me like a man.”
Siku chache baadaye Yeezy alilazwa kwenye hospitali ya UCLA Medical Center kutokana na kuwa na uchovu mwingi.
No comments:
Post a Comment