NUSU FAINALI MAPINDUZI CUP 2017, NI SIMBA AU YANGA ?? JIBU KUPATIKANA KESHO.. ZIJUE TAKWIMU HIZI
Hatimaye yametimia, ni nusu fainali ya Mapinduzi Cup 2017 itakayozikutanisha Simba na Yanga kutafuta mshindi atakaefuzu kwenda fainali ya michuano hiyo inayozidi kushika kasi visiwani Zanzibar.
Magoli mawili ya Laudit Mavugo kwenye mchezo wa Kundi A dhidi ya Jang’ombe Boys yameifanya Simba kufikisha pointi 10 na kuwa kinara wa kundi hilo.
Yanga baada ya kusukumwa goli 4-0 na Azam FC kwenye mchezo wao, wakajikuta wanamaliza katika nafasi ya pili kwa pointi zao sita nyuma ya Azam yenye pointi saba.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, kinara wa kundi A anakutana na mshindi wa pili kutoka Kundi B wakati Kinara wa Kundi B yeye anakutana na timu iliyoshika nafasi ya pili katika Kundi A na hapo ndipo mechi ya Simba na Yanga inapozaliwa.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano, mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuchezwa siku ya kesho Jumanne January 10 saa 2:15 usiku kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Baada ya kusugua benchi kwa muda na kuandamwa na ukame wa kufunga magoli, hatimaye mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo amefunga magoli yote mawili kwenye mchezo dhidi ya Jang’ombe Boys.
Kutokana na muonesha kiwango bora katika mchezo huo, Mavugo alitangazwa kuwa man of the match ambapo alikabidhiwa carton nne za kinywaji cha Malti kutoka kampuni ya Azam.
Peter Manyika Jr ameonesha kiwango kizuri hususan katika mchezo dhidi ya Jang’ombe Boys ambapo aliweza kufanya saves mbili za nguvu wakati wa kipindi cha pili.
Manyika ambaye amekuwa akikaa benchi kwa muda mrefu tangu enzi za Vicent Angban na mechi tatu za raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara tangu alivyowasili golikipa Daniel Agyei kutoka Ghana.
Katika mechi mbili alizoanza za Mapinduzi Cup (Simba 0-0 URA NA Simba 2-0 Jang’ombe Boys, amefanikiwa kucheza dakika 180 bila kuruhusu bao (clean sheets)
No comments:
Post a Comment