PICHA : WATUHUMIWA WA MADAYA KULEVYA WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI LEO NA MAAMUZI YALIYOTOLEWA



Watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi ya leo.. 

Waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imetoa maamuzi ... 


Mahakama hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili Petitman na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 20 na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa muda wa miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.

Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi  watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.