MWANAFUNZI WA SEKONDARI AKAMATWA AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA COCAINE



Wakati vita dhidi ya madawa ya kulevya ikiendelea Dar, imetua pia jijini Mbeya baada ya polisi kutangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa na kete za cocaine eneo la Mbalizi jijini humo

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Dhahir Kidavashari amesema kuwa polisi wamemkamata kijana huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali huku akisema upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.
Amesema vita dhidi ya madawa ya kulevya imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa mtandao unaosambaza dawa hizo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.