TID MNYAMA - " STEVE NYERERE SIO STAR KWANGU NI PANYA "

Image result for tid tanzania

Hivi karibuni, kwenye mazungumzo yaliyovuja kati steven nyerere na mama yake Wema Sepetu, alidai kuwa hitmaker wa Siamini, TID alipewa fedha na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili atoe hotuba kuhusu kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya.
Mnyama alimind mbaya na kutishia kumshtaki mchekeshaji huyo. Na sasa mkali huyo ameibuka na kumwelezea Steve kuwa si staa kwake, bali ni kama panya tu.
“Steve Nyerere sio staa kwangu, he is a mouse,” ameiambia E-News ya EATV.
“Ukimuangalia kwanza he is a mouse, to me, me I have been doing this talent na nimejijengea umaarufu kupitia kipaji changu, sio kupitia uongo uongo, udananda sijui umbea umbea, sijafanya hivyo,” ameongeza.
“I have been working very hard to make this name. Huwezi kuniambia mimi eti nimepewa milioni mbili sijui, unanidhalilisha, kwanza unanihatarishia maisha yangu mtaani mimi nionekane snitch, nimewasnitch wananchi, nimepewa milioni 3 kuconfess pale, why? Milioni mbili na maisha yangu?
TID amemtaka Steve afike mbele ya mahakama athibitishe kuwa alichukua shilingi milioni 2, lasivyo patachimbika.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.