ZITTO AMTAKA RAIS JPM KUVUNJA BUNGE, KAMA ANAONA BUNGE KIKWAZO



Katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kuapishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rais Magufuli amewataka viongozi wengine kumuunga mkono mtu anayejitokeza kupiga vita dawa za kulevya badala ya kumdhalilisha.

"Tunapomuona mtu anajitokeza kupambana na haya madawa ya kulevya, badala ya kumdhalilisha tumuombee na kumtia moyo, hawa wanaweza hata kubadilisha maneno uliyoyazungumza wakabadilisha wakatengeneza kwenye clip wakatupa, na wakajitokeza wengine wakasema wameingilia mamlaka yao, wakati wao wanaingilia mamlaka ya kuwaita wengine, hii ni vita". Amesema Magufuli

Image result for magufuli

Baada ya kauli hiyo ya Rais, Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook ameonesha kushangazwa na kile alichodai  kuwa Rais hakujua kuwa sheria ya kuundwa kwa mamlaka hiyo, ilitungwa, na kwamba anashangaa kuona Rais hakuwa akijua kuwa alipaswa kumteua Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo


" Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi."

"Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya? "

" Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje".

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.