AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA TRENI AKIWA ANAPIGA PICHA ZA MITINDO RELINI

Fredzania Thompson

Mwanamke wa umri wa miaka 19, ambaye alikuwa anaanza kujikuza kama mwanamitindo, aligongwa na treni na kufariki alipokuwa anapigwa picha.
Fredzania Thompson alikuwa anapigwa picha hizo za mitindo, ambazo zilikuwa za kwanza, kwenye reli alipogongwa.
Picha za Thompson, alizopigwa muda mfupi kabla ya mkasa huo kutokea Navasota, Texas, zimesambazwa na familia yake.
Polisi wanasema alikuwa mjamzito wakati huo na kwamba alikuwa anavuka treni moja kwenye njia moja ya reli alipojikuta ameingia kwenye njia nyingine ya reli ambapo kulikuwa na treni nyingine iliyokuwa inapita ambayo ilimgonga.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.