KUTANA NA RITAH, MCHORAJI KIPOFU ALIYEPEWA MEDANI NA RAIS

Blind
Ritah Kivumbi ni mwanamke mahiri katika tasnia ya Sanaa ya uchoraji nchini Uganda ingawa ni kipofu.
Ritha alisema, alipata shida hiyo ya kutoona wakati akiwa mtu mzima, kipindi ambacho alikuwa ameajiriwa kama msimamizi wa nyumba ya sanaa katika chuo kikuu cha Makerere mwaka 2008.
Ilimchukua kipindi cha miaka sita kurudi katika tasnia yake ya sanaa,mara baada ya kugundua kuwa ana uwezo wa kutengeneza hereni.
Msanii huyu anawezaje kuchora wakati haoni?.. hya ndio majibu aliyotoa 
"Kwa sasa nina uelewa wa rangi ninazotaka, uelewa wa rangi hapa ninamaanisha kuwa nikichanganya rangi nyenkundu na njano najua nitapata rangi ya machungwa...na nikitaka rangi ya kijani kibichi najua itanibidi nichanganye rangi ya njano na kijani.
Nina vikopo vyangu ambavyo hutumia huwa naomba msaidizi wangu kunilete vikopo hivyo ambavyo niliweka alama fulani ambazo zinaifahamisha kuwa rangi mbalimbali mfano nikipapasapapasa nitajua kuwa hii ni rangi nyekundu au njano ."
Ritha
Licha ya msanii huyo kufanya anachoweza na kupenda ili kuweza angalau kijipata kipato lakini anakabiliwa na changamoto mkiwemo hufukuzwa kutoka madukani akiwa anaongozwa na binti yake akiuza michoro yake.
Pamoja na changamoto nyingi ambazo anazipitia,Ritha anajivunia kazi yake ni fahari Ingawa wakati fulani pesa huwa shida kupatikana lakini anajivunia kazi yake ambayo pia alipewa medali kutoka kwa rais wa nchi hiyo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.