" SIJALIPWA HATA MIA KUTOKA KWA HARMORAPA, HANA HELA YAKUNIPA " - JUMA NATURE



Msanii Juma Nature amevunja ukimya baada ya Harmorapa kumtuhumu kumdai pesa ya mavazi kwa ajili ya video ya wimbo wake mpya ‘Kiboko Ya Mabishoo’.

Akiongea na kipindi cha E News cha EATV Jumatatu hii, muimbaji huyo amesema rapper huyo chipukizi hana pesa ya kumlipa.
“Nikisema nimemlipisha Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea. Mimi ni mtu mzima nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na imani atafika mbali. Hawezi kunilipa mimi, ana hela gani?,” amesema Nature.
Wiki chache zilizopita, Harmo alimlalamika msanii huyo mkongwe kupitia kipindi hicho kwa kusema, “Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe.”

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.